Nembo ya manispaa ya Furth

Nembo imegawanywa katika sehemu tatu zenye rangi za nyekundu, nyeusi, dhahabu na fedha. Gurudumu linawakilisha mtakatifu Katharina, ambaye ni matakatifu mlinzi wa kijiji cha Arth. Kanisa la huko pia limetengwa maalum kwa ajili ya Mtakatifu Katharina. Upanga unawakilisha Mtakatifu Michael – matakatifu mlinzi wa wilaya ya Schatzhofen. Sio tu wakaazi wanaume pekee wa eneo hili waliorithi jina hili la kwanza bali pia kanisa la parokia. Dubu ndiye mnyama wa nembo ya familia ya Kaergl ambayo iliishi Furth hadi 1615. Kutokea kwao ndio ngome ya ulinzi na kiwanda cha pombe vilitengenezwa.

Kutoka kwa takwimu

SLP: 84095
Vorwahl: 08704
Eneo: Mita 427.242 juu ya usawa wa bahari
Upanuzi wa Eneo: Kilomita 20,94 za mraba
Idadi ya wakaazi 31.12.2022: 3,659
Baraza la Mji: Furth, Am Rathaus 6, Tel.: 08704/9119-0

Umri na Idadi ya watu

Umri wa miaka: 40 Jahre
Walio na hadi miaka 18: 21,3 %
Walio na miaka 18 hadi 64: 63,1 %
Walio na miaka 65 na zaidi: 15,6 %
Ongezeko la idadi ya watu: kutoka 1999 mpaka 2009: 14,1%
Waliozaliwa 2009: 12,4 kwa kila wakaazi 1,000
Vifo mwaka 2009: 9,1 kwa kila wakaazi 1.000
Makaridio: Idadi ya watu katika wilaya ya Landshut inatarajiwa kuongezeka kwa 4,9 % ifikapo 2028. Uwiano wa vijana kwa wazee utabadilika kutoka idadi ya sasa ya 36,8% hadi 27,6% na kufikia 31,8% hadi 41,9%.

Muundo wa mapato:

Pato la jumla kwa mfanyakazi na mlipa kodi ni wastani wa euro 32,868 (Kwa jimbo la Bavaria ni euro 31,891)
Kwa kila wakaazi 1,000, watu 378 huajiriwa kulingana na michango ya huduma za ustawi wa jamiii (mahali wanapoishi) (Kwa wastani Bavaria: watu 355)
Kwa kila watu 1,000, watu 65 huajiriwa kulingana na michango ya huduma za ustawi wa jamii (mahali pa kazi) (Kwa wastani jimbo la Bavaria: watu 361).