Nishati

Manispaa ya Furth ina jukumu la utangulizi katika uzalishaji endelevu, matumizi na uhamasishaji wa nishati mbadala. Pamoja na wananchi, jumuiya inajitahidi daima kupanua jukumu hili la upainia na hivyo kufikia lengo la kujitosheleza kwa nishati uwiano. Lengo kwa sasa ni kuokoa nishati. Hapa tuna nafasi ya kufikia 100% ikiwa kila mtu atasaidia.

Nishati

Kutizama mara moja kunatosha. Kwa taswira ya hali ya ndani ya nishati ya mji wa Furth, Bayernwerk hutengeneza mfumo wa uwazi na mwelekeo kwa miji, masoko na jamii. Chombo cha kusimamia Mabadiliko ya nishati kinaonyesha mkondo sahihi wa mustakabali wa nishati ya eneo hilo. Kinachoonekana kama maono kinaelekea kuwa cha kweli mjini Furth. Furth, Altdorf, na Schrobenhausen ni miongoni mwa manispaa za majaribio ambazo zinatumiwa na Bayernwerk kutengeneza chombo cha kusimamia mabadiliko ya nishati. Kampuni hiyo imewasilisha hali ya maendeleo kwa Meya wa Fürth Andrea Horsche.

Sio siri tena. Mustakabali wa nishati upo mikononi mwa ofisi za mitaa na sio katika ofisi moja kuu. Baada ya awamu ya kwanza ya mustakabali wa nishati kudhihirishwa na upanuzi wa nishati jadidifu, mahitaji ya nishati kwa wateja yanazidi kuunda mustakabali wa usambazaji wa nishati. Zaidi ya hayo, lengo linaendelea kuwa kwa matumizi ya nishati ya kijani kadri inavyowezekana. Kwa hiyo manispaa huwa na mchango mkubwa kama soko la nishati la kesho. Hata hivyo, ongezeko la aina mbalimbali za chaguzi na kasi ya mabadiliko ni changamoto kubwa. Ili kuanza mkondo sahihi, kinachohitajika Zaidi ya vyote ni uwazi kuhusu hali ya nishati ya ndani. “Kwa bidhaa yetu ya kiubunifu na kidijitali, chombo cha kusimamia mabadiliko ya nishati, tunaweza tukatengeneza uwazi huu” Alisisitiza Dkt. Alexander Fenzl, ambaye anahusika na mwelekeo wa kimkakati na maendeleo ya ulimwengu wa bidhaa mpya katika kampuni ya Bayernwerk. Kwa manispaa, bidhaa hii huchangia katika uamuzi wa kozi na hiyo kuongeza thamani yake. Chombo cha kufuatilia gridi ya nishati cha kampuni ya Bayernwerk huchunguza mazingira magumu ya nishati ya ndani kwa wananchi na manispaa.

Kupitia jukwaa linaloweza kutazamwa mtandaoni, kinachojulikana kama dashibodi, chombo hicho cha kuchunguza nishati hutoa tathmini rahisi inayoeleweka ya uzalishaji nishati na matumizi ya nishati ya ndani. Hii huziwezesha manispaa kuamua kuhusu kiwango chao cha kujitosheleza: Kiasi gani cha umeme kinachozalishwa katika jamii hiyo, kiasi gani kinachotumika, na kiasi gani kinachotoka kwenye gridi ya umeme.

Chombo cha kusimamia mabadiliko ya nishati huangazia mazingira ya nishati ya manispaa hiyo. Kwa njia hii, pia tunajenga uwelewa wa hali ya nishati ya ndani miongoni mwa wananchi, ambao ni msingi muhimu katika maendeleo Zaidi. Chaguzi za wazi za hatua ya kuchukuliwa zinaweza kutolewa kwa uazi uliopatikana. Kwa manispaa, chombo hicho cha ufuatiliaji pia ni mfumo wa usimamizi wa utanuni Zaidi wa nishati ya siku za usoni” Alieleza Meya Andreas Horsche. Lengo la Bayernwerk na Soko la Furth ni soko la jumla la nishati ya ndani lenye uwakilishi unaoonekana wa uzalishaji wa nishati binafsi.