Meya wa kwanza Andreas Horsche

Andreas Horsche alizaliwa mwaka wa 1978 katika mji wa Erfurt (Thüringen). Baada ya mafunzo ya useremala na kutumika kwa miaka mianne kama askari wa muda katika kitengo cha muziki jeshini, alisomea utawala katika taasisi ya FHVR mjini Saale. Kabla ya kuchaguliwa kuwa Meya wa kwanza, alifanya kazi kama afisa wa utawala katika mji mkuu wa jimbo la Bavaria, Munich na mji wa Abensberg.

Tangu mwaka wa 2014 amekuwa Meya wa Manispaa ya Furth na pia Mwenyekiti wa jumuiya ya kiutawala yenye jina sawa na hilo pamoja na manispaa nyingine wanachama za Obersüßbach na Weiihmichl.

Meya wa pili Josef Fürst

Josef Fürst alizaliwa 1952 katika mji wa Linden (Arth). Amekuwa mwanachama wa halmashauri ya mtaa wa Further tangu mwaka wa 1978. Mkulima huyu kutoka Arth amekuwa na ushawishi mkubwa katika maendeleo ya mji huo kwa miongo iliyopita. Akiwa kama mwanachama wa chama cha Christian Social Union, ni mjumbe wa baraza la manispaa na mjumbe wa kamati ya ujenzi na mazingira, mwanachama wa baraza la mambo ya utawala, mwanachama wa bodi ya wakurugenzi wa taasisi ya manispaa ya Furth na mwakilishi kwenye baraza la chama cha maendeleo jumuishi ya vijijini. Kwa kipindi cha miaka 2020-2026, Josef Fürst alichaguliwa mara kadhaa kama naibu wa Meya. Kabla ya hapo aliiwakilisha ofisi ya meya wa tatu kwa miaka mingi.

Meya wa tatu Monka Dierl

Monika Dierl alizaliwa Vilsbiburg mnamo mwaka wa 1970 na kukulia katika eneo la Landshut.

Tangu 2008 ni mwanachama wa Halmashauri ya mtaa wa Furth. Msaidizi huyo wa mambo ya matatizo ya kuzungumza, amekuwa na mchango mkubwa kwenye maendeleo ya miaka iliyopita hasa katika kazi za watoto na vijana. Kama mwanachama wa Kundi la wa Wapiga Kura Huru au Free Voters, yeye ni mwanachama wa chama cha muungano wa kampuni ya FuKeE, mjumbe wa Jumuiya ya utawala ya Furth, mwanachama wa jumuiya ya maendeleo ya vijijini huko Holledauer Tor na nmjumbe wa kamati ya ujenzi na mazingira. Monika Dierl alichaguliwa kuwa meya wa tatu kwa muhula wa 2020-2026.