Manispaa Washirika

Manispaa Washirika - Neue Partnerschaft mit Karagwe in Tansania

Katika msimu wa vuli wa mwaka wa 2022, Manispaa ya Furth ilianzisha ushirikiano mpya na Karagwe nchini Tanzania.

Wilaya ya Karagwe kimsingi inalinganishwa na Wilaya ya Landshut. Hata hivyo miundo ya kiutawala inayowezesha ushirikiano wa manispaa inapatikana tu katika ngazi ya wilaya nchini Tanzania.

Ushirikiano wa manispaa kati ya kijiji hicho cha jimbo la Bavaria na Wilaya ya Karagwe una faida nyingi kwa pande zote. Moja ya sababu kuu ni fursa ya kubadilishana uzoefu wa tamaduni mbalimbali. Kwa kubadilishana watu, mawazo na taarifa, pande zote mbili zinaweza kujifunza mengi kutoka kila mmoja na kutanua mitazamo yao. Sababu nyingine muhimu ni fursa ya kufanya kazi pamoja katika changamoto za kimataifa kama vile umaskini, uchafuzi wa mazingira na ukosefu wa haki. Kwa kufanya kazi pamoja, pande zote mbili zinaweza kuunganisha rasilimali na ujuzi wao na kwa pamoja kutengeneza suluhu za kiubunifu. Ushirikiano unaweza pia kusaidia kuboresha mazingira ya kiuchumi na kijamii katika maeneo yote mawili. Kuna njia nyingi za kutekeleza miradi kupitia ushirikiano ambayo inasaidia kuboresha hali ya Maisha, kama vile elimu, afya, biashara, na miradi ya kimazingira. Ushirikiano pia unaweza kusaidia kukuza uelewa wa utamaduni na hali ya maisha ya nchi nyingine na hivyo pia kukuza maelewano na kuvumiliana. Kwa pamoja tulikubaliana toka mwanzoni kuchukua hatua ndogo ndogo katika kazi ya ushirikiano. Inawezekana watu wa maeneo yote mawili kukua katika ushirikiano huo. Tungependa kutafsiri sehemu za tovuti hii katika Kiswahili ili kubpresha taarifa kuhusu Furth na wilaya hiyo ya Tanzania. Zaidi ya hayo, tunataka kujaribu kubadilishana mawazo mara kwa mara. Hii ni Pamoja na uwezekano wa kutembeleana. Hata hivyo, cha muhimu ni kuwa tunataka kuzingatia mada za ulinzi wa mazingira. Hasa uepushaji taka na uchakataji wa taka vinapaswa kuwa lengo la ushirikiano wa manispaa zetu. Katika majira ya machipuko mwaka huu, tunatarajia ziara ya washirika wetu wa Tanzania mjini Fürth. Katika shughuli zote hizi, tunaungwa mkono na SKEW.

Manispaa washirika wa awali

Manispaa ya Furth ilidumisha ushirikiano na Krupski Mlynn nchini Poland, Ottensheim nchini Austria na Breitenbach huko Alsace kupitia ushirikiano na Agenda 21. Kutokana na mabadiliko ya ndani ya kisiasa, ushirikiano huu umesimamishwa kwa muda ukisubiri.