Elimu na malezi - Bildung und Erziehung

Baraza la manispaa kwa makusudi limeipa mada hii kipaumbele mbele kwa sababu Furth ni eneo bora kabisa la elimu.

Nyumba za kuwalea watoto, shule za kawaida, shirikishi na chechekea za msituni, kuwafuatilia watoto wakati wa chakula cha mchana, malezi ya watoto baada ya shule jioni, Shule za msingi na sekondari na shule ya sekondari ya Maristen, kituo cha elimu ya watu wazima cha jamii pamoja na jumuiya za Obersüßbach na Weihmichl, maktaba ya kisasa, madarasa rafiki kwa mazingira karibu na Mto Furth, kituo cha kujifunza na tiba, ni taswira ya elimu ambayo pengine ni ya kipekee kwa ukubwa wa jumuiya hiyo ndogo ya Bavaria.

Kumekuwepo na bado kuna ushirikiano na Chuo Kikuu cha Sayansi cha Landshut, Chuo Kikuu cha Sayansi cha Regensburg, Chuo Kikuu cha Sayansi cha Munich, Chuo Kikuu cha Sayansi cha Weihenstephan na Chuo cha Ufundi cha FOS/BOS Freising. Kazi nyingi za wanafunzi zinahusika na Mkakati Endelevu wa Furth.

Watoto na vijana wenye mahitaji ya utangamano hupewa usaidizi maalum makanisani na taasisi za kijamii kwa mujibu wa dhamira yetu ya jamii jumuishi.

Katika shule yetu ya msingi kuna uwezekano wa kuhudhuria darasa la mjumuisho. Shule ya Msingi ya Furth ilikuwa shule ya kwanza jumuishi katika kanda nzima.

Kazi za vijana katika vikundi vya vijana, na programu za likizo kwa ushirikiano na kanisa, vilabu na vyama huchukua nafasi kubwa. Chama cha Menschenkinder e.V. kinatoa ushauri nasaha na programu ya semina inayofaa kwa familia. Kiwango cha chini mno cha matukio yasiyo ya kawaida ndio malipo ya juhudi hizi za ajabu.

Kwa miaka mingi Manispaa ya Furth imewekeza pesa nyingi zaidi katika elimu na malezi.